16 Julai 2026 - 13:04
Jeshi la Yemen ladai kuidungua droni ya kivita ya Saudi Arabia katika anga la Al-Baydah

Jeshi la Yemen limedai kuwa limedungua ndege isiyo na rubani ya kivita aina ya Wing Loong-2 UCAV inayodaiwa kumilikiwa na Jeshi la Anga la Saudi Arabia katika anga la mkoa wa Al-Baydah nchini Yemen.

Kwa Mujibu wa Shirika la Habari la Kimataifa la Ahlul-Bayt (as) –ABNA– Jeshi la Yemen limetangaza kuwa limeidungua ndege isiyo na rubani ya kivita (UCAV) aina ya Wing Loong-2 inayodaiwa kuwa ya Jeshi la Anga la Saudi Arabia katika anga la mkoa wa Al-Baydah, katikati mwa Yemen.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Yemen, operesheni hiyo ilifanikiwa wakati ndege hiyo ikidaiwa kuwa ilikuwa ikifanya shughuli za kijeshi katika eneo hilo.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa hatua hiyo ni sehemu ya operesheni za kujihami dhidi ya mashambulizi ya kijeshi yanayoendelea nchini Yemen, huku ikisisitiza kuwa vikosi vyao vinaendelea kufuatilia na kukabiliana na ndege na vifaa vya kijeshi vinavyoingia katika anga la nchi hiyo.

Hadi wakati wa kuchapishwa kwa habari hii, hakukuwa na tamko rasmi kutoka Saudi Arabia lililothibitisha au kukanusha madai hayo. Hivyo, taarifa hiyo inabaki kuwa dai lililotolewa na Jeshi la Yemen, huku hali ya usalama katika eneo hilo ikiendelea kufuatiliwa kwa karibu.

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha